Jeshi la Lebanon lagundua kemikali nyingine za miripuko nje ya bandari ya Beirut

Jeshi la Lebanon limesema limegundua tani zaidi ya 4 za madini ya kemikali ya ammonia nitrate karibu na lango la bandari ya Beirut sehemu ambapo ulitokea mripuko mkubwa mwezi uliopita uliosababishwa na mlundiko wa kemikali kama hizo zenye nguvu kubwa ya kulipuka.

 

Kwa mujibu wa tamko la jeshi lililoripotiwa na shirika la habari la serikali, NNA wahandisi wa jeshi la Lebanon wanalishughulikia jambo hilo.

 

Wakati huo huo wanaofanya juhudi za uokozi wamesema wamepata ishara ya kuwepo watu chini ya vifusi vya majengo yaliyoanguka, na hivyo kuleta matumaini huenda wapo watu walionusurika hata baada ya mwezi mmoja tangu kutokea mripuko mkubwa kwenye bandari ya mji wa Beirut.

 

Taarifa hiyo imetolewa na maafisa pamoja na vyombo vya habari mjini humo.Toa comment