Jeshi laahirisha mkutano kuhusu kukabidhi madaraka kwa raia, Mali

2 0

Watawala wa kijeshi nchini Mali wameahirisha mkutano wao wa kwanza uliohusu mpango wa kurejesha madaraka kwa raia baada ya kuongezeka kwa mvutano miongoni mwa viongozi wakuu ambao walisababisha mapinduzi ya Agosti 18.

Wanajeshi waliyaalika makundi ya asasi za kiraia, vyama vya siasa na waasi wa zamani kwa lengo la kufanikisha mashauriano.

Lakini taarifa ya watawala hao wa kijeshi ilieleza kwamba mkutano umeahirishwa katika dakika za mwisho hapo jana hadi utakapotajwa tena kutokana na kile walichosema “sababu za kimaandalizi”.

Kundi la muungano wa waandamanaji ambalo lilikuwa likifanya maandamano dhidi ya Rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keita, linalojulikana kama “June 5 Movement” halikualikwa kushiriki mkutano huo.

Kundi hilo linataka utawala wa kijeshi kuwajibika katika kufanikisha utawala wa kiraia kama ulivyoahidi, pamoja na kutoainishwa muda.

Posted from

Related Post

Mrembo Ajinunulia Jeneza Mil 22

Posted by - October 31, 2019 0
Mrembo Ajinunulia Jeneza Mil 22 October 31, 2019 by Global Publishers KAMA ulikuwa unadhani warembo wa Bongo pekee ndiyo wamefyatuka,…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *