Jezi mpya Man United wazua gumzo

1 0

Miamba ya soka nchini England Manchester United wamezitambulisha Jezi zao za tatu zitakazo tumika msimu wa 2020/21.

Jezi hizo zenye muonekano wa Punda milia zimepokelewa katika mitazamo tofauti na mashabiki wa Mashetani hao Wekundu wa England.

Licha ya baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha United kutumika katika kuitangaza Jezi hiyo akiwemo, Bruno Fernandez, Marcus Rashford na Scott McTominay lakini pia aliyekuwa mchezaji nyota wa klabu hiyo na mfanyabiashara, David Beckham ameonekana kuvalia uzi huo.

Mashabiki wanadai kuwa hazina muonekano mzuri wengine wakisema “Hata Beckham zimemfanya kutokuwa na muonekano mzuri. ” – Mcasemarcus shabiki

Prateek yeye ameandika ” Msajilini Sancho na sisi tuta wasamehe kuhusiana na hiyo jezi yenu ya tatu”.

Luis Parker “Watu wataitumia jezi hii kukatiza Barabarani. ”

Reddevil76 “Kamwe sitaandika jina langu katika jezi hii ya kuzalilisha hatakama nitaipata bure. ” Hayo ni maoni machache katika yale mengi yaliyotolewa na mashabiki wa United.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Posted from

Related Post

Aunt Ezekiel Hana Mimba Yangu

Posted by - September 8, 2020 0
Kusah: Aunt Ezekiel Hana Mimba Yangu September 8, 2020 by Global Publishers Baada ya hivi karibuni kuhusishwa kuwa katika Mahusiano…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *