Jimama la Miaka 42 Mbaroni kwa Kukutwa Likifanya Mapenzi na Katoto

MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 42 nchini Kenya anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa tuhuma za kwa kuanzisha nae uhusiano wa kimapenzi ‘kumbemenda’ na kumbaka mtoto wa kiume anayesoma darasa la nane na kumrubuni amuoe.

 

Mwanamke huyo amekamatwa akijivinjari na mtoto huyo nyumbani kwake Nyamaraga, Kaunti ya Suna juzi Jumaosi jioni ambapo Polisi wanasema walipewa taarifa na Raia wema huku kukiwa na taarifa kuwa anafanya mipango ya kufunga naye ndoa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14.

 

Chifu wa eneo hilo, Evance Nyarube alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa majirani wakilalamika kuhusu uhusiano wa kimapenzi yasiyozingatia umri sahihi. Anasema wamewahi kuwaonya wazazi wa mtoto huyo kuhusu uhusiano huo lakini maombi yao yalikutana na sikio la kufa.

 

“Wazazi wa Mtoto waliwaonya huyu Mama na Mtoto waache hiyo tabia lakini inaonekana mahaba yaliwakolea na wakaendelea kuponda raha,” asema Nyarube. Alieleza kuwa uhusiano huo ni sawa na ubakaji au unyanyasaji wa kingono, hivyo mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria.

 

Mama huyo atafikishwa Mahakama ya Migori, leo Jumatatu, Agosti 31, 2020, kwa kosa la kwenda kinyume cha Sheria ambazo zinakataza kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa kati ya ya miaka 12 hadi 15 na akikutwa na hatia anaweza kukabiliana na kifuongo kisichopungua miaka 20 jela.

 Toa comment