JPM Aanika Siri ya Chenge “Kazi Zipo Nyingi Tu” – Video

13 0JPM Aanika Siri ya Chenge “Kazi Zipo Nyingi Tu” – Video

 

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli amemweleza aliyekuwa mbunge wa Bariadi Mkoa wa Simiyu, Andrew Chenge kuwa asiwe na wasiwasi kwa kukosa ubunge kwani bado kuna vyeo vingi Serikalini.

 

Magufuli amesema hayo leo, Agosti 4, 2020, wakati akiendelea na kampeni za kuwania nafasi hiyo na kuwatambulisha madiwani na wabunge wa chama hicho katika mji wa Bariadi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika Oktoba 28, mwaka huu.

 

Baadhi ya kauli muhimu alizotoa Magufuli katika hotuba yake ni:

“Nimezungumza Shinyanga na maeneo mengine, kazi zipo nyingi, Mzee Chenge ‘Mtemi’ ni kaka yangu kwelikweli, nilipoingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1995 mke wangu alikuwa na mimba, aliyenisaidia pesa za kwenda hospitali ni Chenge, huu ndiyo ukweli.

 

“Mhe. Chenge kazi zipo nyingi mno hata utemi nao ni kazi kubwa tu, Bariadi achaneni na maneo ya upinzani, leo nataka niwaite wote watatu; Andrew Chenge (Bariadi), Dkt. Chegeni (Busega) na Salum Mbuzi (Meatu) waniombee kura hapa. Njooni hapa wote,”  Dkt. Magufuli.

 

“Akizungumza baada ya kuitwa na Magufuli, Chenge amesema; Mhe. Rais nakushukuru sana, sikutegemea kama histioria hiyo ya mwaka 1995 ungeisema mbele ya wananchi hawa, nakushukuru sana na ninamshukuru Mama Janeth kwa moyo wake wa upendo.

 

“Tutahakikisha tunapata ushindi mkubwa wa kura zako, namhakikishia kijana wetu Injinia Kundo, mimi na Komando Suzy tutafanya kazi ya uhakika kuhakikisha kura za mbunge zinatosha, za madiwani 31 zinatisha, japo tayari madiwani wamepita bila kupingwa lakini hatubweteki.

 

“Mhe Rais wewe ni mtemi wa Tanzania, tunatekeleza tu matawaka ya katiba, isingekuwa hivyo basi tayari wewe ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Umeitendea haki Simiyu na Tanzania,” amesema Chenge.

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *