JPM Amteua Brig. Jen. Mbungo Kuwa Mkurugenzi Takukuru – Video

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Brig. Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo baada ya kuokoa Shilingi Bilioni 8.8 za wakulima.

 

Rais Dkt. Maguguli Amechukua uamuzi huo baada ya kupokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mapema leo katika Ikulu ya Chamwino Jijini, Dodoma.

 

“Kaimu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brig. Jen. Mbungo kuanzia leo nakupandisha nafasi kuwa Mkurugenzi, unafanya kazi nzuri, umeokoa Tsh bil. 8.8 walizodhulumiwa wakulima, ila kuna wachache wa hovyo kama yule wa Kinondoni na wenzake 4, namfahamu na anayofanya,” amesema Rais Magufuli.

 
Toa comment