jpm: “Wanafikiri Nitaahirisha Uchaguzi Sababu ya Corona?” – Video

Rais Dkt. John Magufuli amesema uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautaahirishwa licha ya kuwepo kwa tishio la mlipuko wa virusi vya corona (COVID-19).

 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Machi 26 Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ripoti ya Takukuru.

 

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakifikiri kwamba kazi hazifanyiki na hakuna kukutana kwa sababu ya corona. Amesema hata nchi zilizoathirika zaidi na virusi hivyo, bado mabunge yao yanakutana kama kawaida.

 

“Hatujazuiliwa kukutana, sisi tunaendelea kukutana na tunakutana katika mikutano ya kawaida, na uchaguzi tutafanya tu, wako wengine wanafikiri nitaahirisha, nani anataka kukaa kwenye maofisi muda wote huo?” amehoji Rais Magufuli.

 

“Leo nilikuwa nasoma gazeti moja linasema Madiwani wafanya kikao sijui alifikiri wamezuiliwa kukutana kwa sababu ya Corona? Sisi tunaendelea kukutana, hata nchi zilizoathirika, bado mabunge na mabaraza hayajafungwa,” amesema Rais Magufuli.

 
Toa comment