Julio: Wapeni Muda Yanga, Watakaa Sawa

KOCHA wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefichua kuwa kwa jinsi kikosi cha Yanga kilivyo msimu huu itachukua muda kuwafikia wapinzani wao Simba.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Julio alisema: “Ukiangalia Simba tayari wameshakaa muda mrefu wakiwa pamoja na hata ukiangalia walivyocheza kwenye Ngao ya Jamii tayari walikuwa wakicheza kitimu tofauti na Yanga ambao bado wanajenga timu yao kutokana na wachezaji wengi kuwa wapya.

“Ukweli itawachukua muda kukaa sawa ili kuweza kwenda na kasi ya ligi lakini Yanga pia kocha anatakiwa kuwa makini katika ubadilishaji na upangaji wa kikosi, angalia mtu kama Kaseke (Deus) hakupaswa kucheza muda mrefu ila alikosea kumtoa Farid (Mussa) maana alikuwa katika kiwango bora,” alisema Julio.

Waandishi: Julius Richard, Christopher Mabula na Karim Mohamed.

Pakua App ya Global kwenye Google Playstore, App Store. Utasoma Habari, Magazeti yote kutoka GPL

⚫ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫ iOS:https://apple.co/38HjiCxToa comment