Juma Abdul Kurejea Yanga?

 

Beki wa zamani wa Yanga, Juma Abdul amesema kwa sasa anafikiria zaidi kucheza soka la kulipwa na kuna dili analisubiri na kama likitiki tu anasepa.

 

Beki huyo mtaalamu kwa krosi maridadi amesema kwa sasa hajasaini timu yoyote hapa nchini labda dili lake la kwenda nje likwame ndipo anaweza kufikiria timu nyingine ya kwenda.

 

Abdul pamoja na beki mwingine wa kati, Kelvin Yondani walitangazwa kuachwa na Yanga klabu ambayo waliitumikia kwa miaka nane. Ilidaiwa Yanga iliachana na wachezaji hao kwa madai ya kushindwana katika maslahi.

 

Hata hivyo ndani ya siku mbili hizi kumeibuka maneno kuwa klabu hiyo imepanga kuwaita tena mezani wachezaji hao wazoefu ili kufanya nao mazungumzo ya kuwemo katika kikosi hicho msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.Toa comment