Jurgen Klopp amkataa Messi asema hakuna uwezekano wa nyota huyo kujiunga na Liverpool

4 0

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa Leonel Messi hatajiunga na Liverpool, ingawa amekiri kuwa litakuwa jambo ‘zuri’ kujiunga na ligi ya Primia.

Mustakabali wa Messi umezungukwa na hisia na tetesi tangu alipoomba kuondoka Barca.

Alipoulizwa kama ana mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 33, Klopp alosema: “Nani asiyemtaka Messi kwenye timu yake? Miaka sio tatizo kwetu, lakini kwakweli ni mchezaji mzuri.”

Klopp ameulizwa kama angependa kumsajili mchezaji huyo, 33, Klopp amesema: ”Nani hamhitaji Messi kwenye timu yao?

Jurgen Klopp and Lionel Messi

Messi amekuwa akihusishwa na taarifa za kwenda kuungana na kocha wake wa zamani Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City- kitu ambacho Klopp amesema ”ni wazi” itawasaidia mahasimu wake kuwafanya kuwa ”wagumu kufungwa”.

City waliokua wapinzani wa karibu wa Liverpool msimu uliopita huku wakiwa mabingwa watetezi, wamekua mstari wa mbele katika fununu hizo huku wakiwa tayari kuwaachia wachezaji wake wa kikosi cha kwanza Bernardo Silva, Riyad Mahrez na Gabriel Jesus ili kubadilishana na Messi.

Kwa ligi ya primia, itakuwa vyema, lakini sina uhakika kama ligi ya primia inahitaji usaidizi huo,”aliongeza Klopp.

”Hajawahi kabisa kucheza kwenye ligi nyingine. Mpira wa miguu ni tofauti hapa. Ningependa kuona hilo lakini sina uhakika kama nitalishuhudia,” alisema Klopp.

Chanzo BBC.

Posted from

Related Post

Rose: Sasa ni Wakati wa Ndoa

Posted by - March 7, 2020 0
Rose: Sasa ni Wakati wa Ndoa March 7, 2020 by Global Publishers MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *