Juventus wamfungia kazi Pogba – Gazeti la Dimba

20 0


TURIN, ITALIA

KLABU ya Juventus bado imeendelea kufukuzia saini ya kiungo
wa Manchester United, Paul Pogba, huku ikitaka kumalizana naye kabla ya dirisha
la usajili nchini Italia halijafungwa mwanzoni mwa mwezi ujao.

Nyota huyo alikuwa akitakiwa na matajiri Real Madrid ambao
walishindwa kufika dau la Pauni milioni 180 ambalo linatakiwa na United.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Calciomercato cha nchini
Italia, Juve haijaachana na mpango wa kumrejesha nyota huyo wa kimataifa wa
Ufaransa ambaye amewahi kukipiga katika timu hiyo.

Wote wawili, Pogba na wakala wake Mino Raiola, wameweka wazi
kuwa kiungo huyo anataka kuondoka kwa mabingwa mara 20 wa taji la Ligi Kuu ya
England.

Hata hivyo Mashetani Wekundu ambao watafungua pazia la Ligi
Kuu England dhidi ya Chelsea leo wameshindwa kufanya usajili wa kiungo mwingine
wa kati katika dirisha la usajili lililopita.


Source link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *