Kagere Apigwa Stop Kurejea Simba

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere atachelewa kurejea nchini kufuatia Shirika la Ndege la RwandAir kufuta safari zake zote kwa muda wa siku 30 kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona.

 

Kagere anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa na amefunga jumla ya mabao 19 katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara akifuatiwa na Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar, Paul Nonga wa Lipuli na Relliants Lusajo kutoka Namungo ambao wote wana mabao 11 mpaka sasa.

 

Taarifa iliyotolewa juzi Jumapili na shiriki hilo ambalo lina ratiba nyingi za kuingia nchini, ilisema kuwa imeamua kufuta safari zake zote kwa muda wa siku 30 kutokana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo kufuatia kuwepo kwa ugonjwa huo.

“Kutokana na taarifa iliyotolewa na Wizara Afya ya Rwanda juu ya mlipuko uliokumba dunia kupitia Ugonjwa wa Covid-19, Shirika la RwandAir linafuta safari zake zote kwa muda wa siku 30 kwa ndege zote.

 

“Wateja wote waliokuwa wamekata tiketi wana njia nyingi za kufanya ikiwemo kukata tena kwa ajili ya safari za mbeleni na ada ya makato itaondolewa,” ilisema taarifa hiyo.

 

Championi Jumatano lilimtafuta mshambualiaji huyo ambaye alisema kuwa suala la kurejea nchini litategemea hali ya ugonjwa huo itakavyokuwa kutoka kwenye mamlaka husika.
Toa comment