Kajala Amtaja Shetani Bifu na Wema!

MWANAMAMA mkali mbele ya kamera za Bongo Movies, Kajala Masanja, amesema kuwa, alijua tu kwamba angepatana na mwigizaji mwenzake, Wema Isaac Sepetu, kwani kila mmoja ana mapenzi ya dhati kwa mwenzake na yaliyotokea ni mambo ya kishetani tu.

 

Kajala ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, japokuwa waligombana kwelikweli, lakini alijua wazi ipo siku wangepatana na kuweka mambo sawa kwa sababu ni marafi ki wa muda mrefu na wameshafanyiana mambo makubwa mno.

 

“Najua wazi mimi na Wema tunapendana sana na tusingeweza kuishi hivi hadi milele kwa sababu kuna wakati mtu anaongea tu pengine kwa hasira, lakini ukweli ni kwamba, mambo yangekuja kuwa mazuri tu,” anasema Kajala na kusisitiza kuwa, amefurahi kupatana na rafi ki yake huyo wa kitambo.

 

Kajala na Wema wameishi kwenye bifu kwa zaidi ya miaka mitano sasa, chanzo kikidaiwa ni kusalitiana kwenye mapenzi, ambapo ilidaiwa Kajala kuchepuka na mpenzi wa Wema.

STORI: IMELDA MTEMA, DARToa comment