Kambi Mpya Yanga Usipime Kigamboni – Picha zipo Hapa

1 0Kambi Mpya Yanga Usipime Kigamboni – Picha zipo Hapa

TIMU ya Yanga imeamishia kambi yake eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam kwenye majengo maarufu ya Avic yaliyojitenga na yenye utulivu mkubwa na vifaa kibao vya michezo ukiwemo uwanja wa ndani kwa ndani na hakuna mgeni anayeruhusiwa kuingia ndani bila ruhusa maalumu.

Timu hiyo inasemekana wameamishwa makazi kutoka katika Hoteli ya Regency Park, Mikocheni na Bilionea wa GSM, Ghalib Mohamed ili wapate maandalizi yenye utulivu tayari kwa kuanza msimu mpya.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya Yanga, tajiri huyo ameamua itakuwa inaishi hapo kuanzia sasa na hakuna habari ya hotelini tena kwani hapo ni pazuri zaidi na kocha amepakubali.

Ukifika eneo hilo unakutana na ukuta mrefu na ndani yake tena kuna ukuta mwingine uliopishana kama nusu kilomita na ndani ya ukuta wa pili ndio kuna majengo mbalimbali ya makazi mapya ya Yanga.

Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic amesema timu hiyo inahitaji angalau mwezi mmoja ili icheze kwa kiwango anachotaka huku akiwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.

Zlatco alisema wachezaji wake katika kilele cha wiki ya Mwananchi,walijitahidi ingawa bado hakuna muunganiko na wataitumia wiki moja iliyobaki kurekebisha mapungufu kabla ya kuanza kwa Ligi Septemba 6.

“Ninachowaahidi hapa kwangu ni kazi na nidhamu, huo ndio mwongozo wangu,” alisema Zlatko na kuongeza, Yanga inahitaji mazoezi zaidi ili kutengeneza muunganiko mzuri na icheze kwa ubora mkubwa.

“Si kazi rahisi kupata muunganiko wa timu kwa muda mfupi hivi, ukizingatia timu ina wachezaji 14 wapya, hivyo inahitaji muda ili kuzoeana.

“Licha ya kwamba muda ni mfupi, tutatumia wiki moja iliyobaki kuyafanyia kazi mapungufu yetu ili tuanze vizuri ligi, lakini ili timu icheze kwa ubora wake inaweza kuchukua mwezi mzima ili kuwafanya wachezaji wote kuzoeana na kucheza kwa maelewano,” alisema Zlatko.

“Nimewaangalia wachezaji wote waliosajiliwa wana vipaji vikubwa, hivyo muhimu wanatakiwa kujitoa kwa ajili ya timu na kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja,” alisema Zlatko.

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *