Kauli ya Tizeba Kwa Shigongo Yashangaza -Video

1 0Kauli ya Tizeba Kwa Shigongo Yashangaza -Video


“Mambo makubwa yaliyofanyika Buchosa kwa miaka mitano tunasema asante sana Mhe. Rais, umetupatia Hospitali ya Wilaya, sasa kazi yako Shigongo tekeleza, songa mbele, wananchi wa Buchosa tumpe kura Shigongo, wafuasi wa Tizeba mliokuwa mnanuna ole wenu niwaisikie.”

Hii ni kauli ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Buchosa aliyemaliza muda wake Charles Tizeba ambayo iliwafanya wengi kushangazwa naye kwa jinsi alivyoonesha ukomavu wa kisiasa
Tizeba alienguliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ‘CC’ na Eric Shigongo kupitishwa baada ya wawili hao kufungana katika kura za maoni jambo ambalo lilihisiwa na wengi lingemfanya kada huyo wa chama kununa.


Kinyume na matarajio hayo ya wengi Tizeba aliibuka na kauli hiyo ya kushangaza ambayo ilizua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii.

“Jamaa kamrahisishia kazi Shigongo, binafsi sikuwahi kuwaza kama Tizeba anaweza kuwa na busara za kiwango cha juu namna hii.”

“Inawezekana kaambiwa atapelekwa kuwa balozi si umemsiki mzee wa nchi (Rais John Magufuli) kasema akishinda anazo kazi nyingi.”

“CCM oyeeeee, Tizeba oyeeee, Shigongo safiiiii.”
Hizi ni baadhi ya komenti za watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii baada ya video ya tukio la Tizeba kumuunga mkono Shigongo kusambazwa.

Hata hivyo kwa upande wake Shigongo alisema kuwa atakuwa mbunge wa watu wote waliomuunga mkono na wale wasiomuunga na kusema kuwa kilichotokea kwenye mchakato wa kura za maoni ilikuwa ni demokrasia na wala siyo uadui.

“Ndugu zangu wana Buchosa nawaomba tuwe kitu kimoja, makundi tuyavunje ili tupate ushindi wa kishindo, baadaye tulete maendeleo kwenye jimbo letu.

“Hatuwezi kushinda tukiwa tumegawanyika, hatutapata maendeleo tukibaguana,” alisema Shigongo kwenye moja ya mikutano yake jimboni Buchosa.

Tizeba na Shigongo walifungana kwenye kura za maoni ndani ya CCM kwa kila mmoja kupata kura 354 ambapo Rais Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa CC alisema waliengua jina la Tizeba baada ya kubaini kuwa alikuwa mmoja kati ya wajumbe waliokuwa na sifa za kupiga kura hivyo kupata nafasi ya kujipigia.

“Katika kura hizo walizofungana ukiitoa kura moja aliyojipigia Tizeba mshindi anakuwa ni Shigongo, hii ndiyo kanuni tuliyotumia,” alisema Rais Magufuli wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Bukokwa, mkoani Mwanza hivi karibuni.Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *