Kauli Ya Tshishimbi Yanga Hii Hapa, Aitaja Simba

17 0

Kauli Ya Tshishimbi Yanga Hii Hapa, Aitaja Simba

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Mkongomani Papy Tshishimbi, ametoa kauli ya matumaini Jangwani kwa kutamka kuwa bado mchezaji halali wa timu hiyo huku akiwaambia hakuna chochote kinachoendelea kati yake na watani wao Simba.

 

Kauli hiyo aliitoa jana baada ya tetesi nyingi kuzagaa mitandaoni kuwa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.

 

Hiyo imekuja ni baada ya kushindwa kufikia muafaka mzuri na viongozi wa Yanga katika kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kwenye timu hiyo.

Akizungumza hilo, Tshishimbi alisema kuwa Wanayanga waachane na maneno ya mitandaoni, yeye bado hajasaini kokote iwe Yanga au Simba.

 

Tshishimbi alisema kuwa, amepewa mkataba na viongozi wa Yanga kupitia wadhamini wao GSM ambao bado hajausaini na kuurejesha kwa viongozi baada ya kushindwana kwenye dau la usajili.

 

Mkongomani huyo anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji, alisema kuwa bado mazungumzo yanaendelea kati yake na viongozi wa Yanga huku akitoa nafasi kwa timu nyingine zitakazomuhitaji kuzungumza naye.

 

“Nawashukuru Wanayanga kwa ushirikiano mkubwa ninaoendelea kuupata, kingine niwaambie kuwa wasifuatilie mambo ya mitandaoni, mimi siyajui hayo mambo ya kuondoka Yanga, wanatakiwa kufahamu kuwa bado nina makataba na timu yangu ninayoichezea, binafsi bado nina furaha ya kuwepo hapa na Mungu akipenda nitaongeza mkataba.

 

“Nafahamu Wanayanga wana hofu ya mimi kwenda Simba, naomba wawe na amani, kikubwa wanachotakiwa kuwa na mawasiliano na mimi kwa kila kitu watakachokisikia kwa kunipigia simu kuniuliza na siyo kuniongelea vibaya. “Bado naitamani Yanga, kama viongozi wakizungumza vizuri na mimi nitabakia hapa, kama sehemu unapata kitu kizuri utawezaje kuondoka, wao waje tuongee.

 

Naomba tuwe pamoja ligi bado haijaisha na kingine nimeshacheza sana Afrika kwangu naona muda muafaka wa kwenda Ulaya kama nikiondoka hapa,” alisema Tshishimbi. Aidha, Spoti Xtra limepata taarifa kuwa, kiungo huyo ametaka dau la Sh Mil 150 ili aongeze mkataba wa kuendelea
Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *