Khaligraph Jones apagawa na kipaji cha msanii Adasa Kenya!

3 0

Msanii na rapper mkali Africa kwasasa Khaligraph Jones kutoka Kenya amezua gumzo mtandaoni baada ya kushindwa kujizuia na kufunguka hadharani kupitia mtandao wa Instagram jinsi anavyomukubali msanii wa muziki wa kizazi kipya Adasa.

Adasa ambaye kwasasa anatamba na kibao chake kipya alichoshirikishwa na rapper Benzema wa Kenya pia kwa jina Najikakamua, anauwezo mkubwa wa sauti na amekua akitikisa mawimbi ya radio na televisheni nchini Kenya kwa mUda sasa. Japo wasanii wengi wamekua wakimkubali nyota huyu anaibuka kwa kasi, ila hakuna hata mmoja ameibuka kumkubali na wengi wamekua wakimchukulia poa.

“Wale wanasemanga Kenya Hakuna Talent, This lady Has one of the Best Voices in Africa and Probably the Best voice In East Africa, Tusibishane Tafadhali, This song is beautiful, Her name is @officialadasa , Kama kitu Ni noma , ni noma #respecttheogs,” aliandika Khaligraph Jones kupitia Instagram yake.

Wasanii kama Prezzo, Sauti Sol, Magix Enga na wengine wengi wamekubaliana moja kwa moja na kauli ya OG kua Adasa anakipaji cha kipekee na huenda akawa hana mpinzani si hapa Africa mashariki pekee bali Africa nzima kama alivyonukuu Khaligraph Jones akitoa hisia zake za ndani. Kupitia instagram Khaligraph Jones amejitoa kimasomaso kuzi pandisha kazi mbili za Adasa “” Tunaendana” na hii mpya kwa jina Tujikakamue aliyomshirikisha rapper mkali Benzema wa Kenya

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *