Kicuya Aahidi Balaa Namungo

Mshambuliaji mpya wa Namungo FC, Shiza Kichuya anasema bado ana matumaini ya kurejea kwenye kiwango cha juu kama ilivyokuwa zamani.

 

Kichuya amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Ruangwa mkoani Lindi akitokea Simba, anasema kikubwa ni kijituma na kufanya mazoezi kwa bidii.

 

“Naamini kuna wachezaji wazuri zaidi ndani ya Namungo, hivyo natakiwa kupambana ili kumwaminisha kocha na kunipatia nafasi ya kila mara kucheza kwenye kikosi cha kwanza.”

 

“Namungo ni timu kubwa ndio maana nimekuja huku, nikifanikiwa kupata namba kila wakati naamini kila mmoja atafurahi kwa kile nitakachokifanya uwanjani,” anasema Kichuya.

 

Mshambuliaji huyo ameongoza kusema licha ya mkataba wake kumalizika ndani ya Simba lakini ukosefu wa namba umechangia kuondoka kwake.Toa comment