Kigwangalla Akoleza Tena Bil 20 za Simba ‘Mo Dewji Alileta Uswahili’

Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema hana tofauti wala chuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kama ambavyo wengi wanavyofikiria baada ya kuhoji juu ya uwekezaji wake wa Tsh bilioni 20.

 

Weekend iliyopita Kigwangalla alizua mijadala katika mitandao ya kijamii muda mchache baada ya kutangazwa kwa mtendaji mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez ambaye ametwaa nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingiza aliyetimkia Yanga Sc.

 

Akitolea ufafanuzi, Kigwangalla amesema; ”Sina matatizo na Dewji, yule ni rafiki yangu na pia alikua mbunge mwenzangu, nilishafanya naye biashara, suala la mkopo wa pikipiki wala sio tatizo kwa kuwa nilimkopa, lakini alileta uswahili, mwanzo alikubali, baadaye alikataa.

 

“Lakini baadaye nilinunua kwa kuwa nilikua nataka kupeleka jimboni kwango ili kukimbizana na muda, hivyo kama ningekua na chuki naye basi nisingerudi tena kununua bidhaa kwake.

 

“Suala la kuhoji Tsh bilioni 20 nilishawahi kufanya hivyo tangu mwezi Januari, hivyo baada ya kuona mambo kama hayaendi vile inavyotarajiwa, ilibidi niulize kwa kuwa niliona wanamuajiri Barbara ambaye ni mfanyakazi kutoka Taasisi ya Mohamed Dewji, maana yake hapo kutakua na tatizo kwa kuwa mchakato haujakamilika.”

 

Kigwangalla amesisitiza kwamba baada ya kuona baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba Sc wamekasirika wakiamini anataka kumfukuza mwekezaji wao, sasa atakaa kimya ila ukweli utakuja kujulikana.Toa comment