Kijana wa miaka 21, abuni zaidi ya ‘Emojis’ 350 zenye asili na utamaduni wa Kiafrika 

21 0

Kutana na O’Plerou Grebet, ambaye amebuni zaidi ya ’emojis’ 350 zenye asili na tamaduni ya Kiafrika ambazo mtu anaweza kuzipakuwa ‘downloadable’ na kuamua kutumia.

O’Plerou Grebet mwenye umri wa miaka 21, kutokea nchini Ivory Coast ni mwanafunzi ambaye anasomea ‘3D design and virtual reality’ ili kumwezesha kupata njia nzuri zaidi katika kazi yake hasa kutambulisha heshima ya Mwafrika na tamaduni zake.

Kijana huyo amezipatia jina ’emojis’ hizo kama ‘Zouzoukwa African emojis’, kwa wale wanaotumia simu janja za Smartphone, kompyuta na baadhi ya vifaa vingine vya aina hiyo basi si wageni katika kukutana na ’emojis’ na pengine hata kuzitumia ambazo huwa zinatoa tafsri ya kitu ama jambo fulani.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *