Kimnana Aeleza Ugumu Kulea Bila Mwanaume

VIDEO Queen maarufu Bongo, Lilian Kessy ‘Kimnana’ amesema kuwa katika maisha yake, hakuwahi kuwaza kuwa single mama, lakini kumbe kuna wakati lazima ukubali kuwa unachopanga wewe hakiwi.

 

Mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mama wa binti mmoja aitwaye Sky, amesema wanaume wana mambo mengi mpaka inafikia hatua unaona bora ulee mtoto wako mwenyewe.

 

“Kusema kweli sijawahi kuwaza kuwa single mama, lakini ndiyo imetokea. Asikwambie mtu, kulea mtoto peke yako ni kazi sana, lakini Mungu mwema maisha lazima yaendelee,” alisema Kimnana.

 

Japo mwenyewe hakutaka kuzungumzia lakini inadaiwa kuwa, bibie huyo ameachana na mzazi mwenzake, Tony Albert ambaye pia ni mtangazaji wa EATV.

STORI Memorise RichardToa comment