Kitilya na Wenzake Walipa Bil 1.5, Waachiwa Huru

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga amewafutia Mashtaka yote Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushauri wa Uwekezaji na Upatikanaji wa Fedha, Harry Kitilya na wenzake wanne baada ya makubaliano ya kuwabakizia shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Dola milioni sita.

 

Kitilya ambaye aliwahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), watuhumiwa wenzake ambao ni Maafisa wa Benki ya Stanbic, Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana wameachiliwa huru baada ya kulipa faini ya shilingi bilioni 1.5 walizotakiwa kulipa na mahakama.

 

Juzi, Kitilya na wenzake walikiri makosa na wametakiwa kulipa TZS 1.5 bilioni kama fidia kwa kuisababishia hasara Serikali na kila mmoja kulipa faini shilingi milioni 1 ya mahakama au kwenda jela miezi sita, kutokana na kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabiri

 

Mashtaka yote 58 yalifutwa  na kubakiza shtaka moja la kuisababishia hasara serikali. Hukumu hiyo ilifanyika katika Mahakama ya Mafisadi.

 

Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka benki ya Standard ya Uingereza.

 

Aidha, walidaiwa kula njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ili waweze kujinufaisha wenyewe na washirika wao. Mawakili wa washtakiwa walikuwa ni Alex Mgongolwa na Jeremiah Mtobesya.

 

Soma zaidi ==> Mahakama Yawafutia Kesi Bosi wa TRA na Wenzake

Soma Zaidi ===> Kigogo TRA, Miss Tz Wafutiwa Shtaka la Utakatishaji Fedha

Soma zaidi ===> Shahidi wa Serikali Akana; “Sijui Chochote Kuhusu Kesi ya Kitilya”Toa comment