KMC Kuanza na Majembe Mapya 11

TIMU ya KMC yenye maskani yake Kinondoni itaanza msimu wa 2020/21 ikiwa na maingizo mapya 11 ndani ya kikosi cha kwanza baada ya kufanya maboresho wakati wa dirisha la usajili.

 

Kwenye usajili uliofunguliwa Agosti Mosi na kufungwa juzi, Agosti 31, KMC iliweza kufanya usajili wa wachezaji hao 11 ikiziba mapengo ya wachezaji wake walioondoka ikiwa ni pamoja na Ramadhan Kapera, Jonathan Nahimana na Charlse Ilanfya.

Wachezaji hao wapya ni Raheem Sheikh, kipa kutoka Mbao FC, Masoud Abdalah,(Dondola) kipa akitokea Coastal Union, Kenneth Masumbuko kutoka Lipuli FC.Reliants Lusajo mshambuliaji kutoka Namungo FC, David Brayson beki kutoka Gwambina FC.

 

Beki Lusajo Mwaikenda kutoka Azam FC, Israel Patick kutoka Alliance, kiungo, Masoud Abdallah akitokea Azam FC. Martin Kigi kutoka Klabu ya Alliance FC, David Mwasa kutoka Lipuli.Andrew Vincent, ’Dante’beki kutoka Klabu ya Yanga.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es SalaamToa comment