Kocha Simba Awapiga Mkwara Yanga

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema malengo makubwa kwenye mechi zake za Ligi Kuu Bara ni kukusanya pointi katika kila mchezo zitakazompa taji la ligi ambalo lipo mikononi mwake.Mbali na hilo, pia kuifunga Yanga ambao ni watani wao wa jadi lipo akili mwake.

 

Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema maandalizi ya msimu mpya yamekuwa mafupi ila hiyo sio sababu ya kupoteza mechi ligi ikianza, anahitaji pointi tatu katika kila mechi.

 

“Nahitaji kuona kikosi kinapata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zote bila kujali tunacheza na nani. Unajua malengo yetu makubwa ni kuchukua kila taji lililo mbele yetu na ili kufi kia malengo hayo lazima tushinde.

 

“Kwenye Ngao ya Jamii mbele ya Namungo hesabu zetu zilikuwa ni kushinda na hata kwenye ligi tunahitaji kushinda, hakuna namna lazima tupambane kufi kia malengo,” alisema.Toa comment