Kocha Sven afunguka kuhusu Kagere

2 0

Kocha wa Klabu ya Simba, Sven Ludwig Vandenbroeck amesema kuwa hana tatizo na mchezaji wake Meddie Kagere kama inavyodaiwa.

Sven amesema kuwa hawezi kutumia nguvu katika mambo yasiyokuwa na maana na wala asiyojua asiyojua yanapotokea.

“Siwezi kutumia nguvu kwenye mambo yasiyo ya maana ambayo sijui yanatoka wapi. Mimi sina tatizo, Medie hana tatizo hilo ndilo ninaweza kusema.”- Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck

Kumekuwa na taarifa zinazoenea kuwa kocha huyo Mbelgiji na mshambuliaji wake Meddie Kagere hawana maelewano mazuri jambo ambalo kwa upande wake amelikanusha.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *