Kocha wa Arsenal na Mchezaji wa Chelsea Wakutwa na Corona

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta.

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekutwa na virusi vya ugonjwa wa corona na mechi kati ya timu yake na Brighton iliyotarajiwa kuchezwa wikiendi imeahirishwa.

 

The Gunners wamefunga uwanja wao wa mazoezi na wafanyakazi waklabu hiyo ambao waligusana na Arteta wamelazimika kujiweka karantini.

 

Ligi ya Premier itafanya mkutano wa dharura na klabu zote siku ya Ijumaa ili kuzungumzia kuhusu mechi zinazotarajiwa kuchezwa.

Mchezaji wa Chelsea Callum Hudson Odoi.

”Hii kwa kweli inasikitisha”,  alisema raia wa Uhispania Arteta mwenye umri wa miaka 37.

”Niliamua kupimwa baada ya kujihisi vibaya lakini nitarudi kazini mara tu nitakaporuhusiwa kufanya hivyo”.

 

Wakati huohuo mchezaji wa Chelsea Callum Hudson Odoi pia amepatikana na virusi vya Corona .

 

”Wachezaji wote wa Chelsea waliogusana naye kikiwemo kikosi chote cha wachezaji 11, wafanyakazi pamoja na wakufunzi sasa watahitajika kujiweka karantini kwa kipindi cha siku 14” , ilisema klabu hiyo ya ligi ya Premia.

Licha ya kupatikana na ugonjwa huo callum anaendelea vyema na anatarajia kurudi katika uwanja wa mazoezi atakaporuhusiwa, ilisema taarifa ya klabu hiyo.
Toa comment