Kumbe Jide Alikuwa Rapa!

 

MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide, amefunguka kuwa mwanzo kipindi anaanza muziki, hakujua kama yeye ni muimbaji.

 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Jide amesema kuwa, alikuwa ni msanii wa kurap na si kuimba japo kipindi cha nyuma alikuwa akiimba kanisani kwenye kwaya na hakujua kama iko siku atakuja kuimba.

 

“Tangu nikiwa kidato cha kwanza, niligundua kuwa najua kurap, sikujua kama nitakuja kuwa muimbaji, japo nilikuwa naimba kwaya kanisani kipindi cha nyuma sana nikiwa mdogo,’’ alisema Jide.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, RISASIToa comment