Kwa Huyu ‘Mtoto’ Kocha wa Yanga Ana Kazi!

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze ana wakati mgumu wa kuangalia mfumo utakaofaa kama atahitaji kumtumia kiungo mshambuliaji mpya, Carlos Stenio Fernandes Guimares ‘Carlinhos’.

 

Yanga imemsajili kiungo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Angola bila kuweka wazi muda wa mkataba walioingia nae na anatarajiwa kuingia nchini leo.

 

Cralinhos anaungana na viungo wengine kama Haruna Niyonzima, Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Deusi Kaseke, Mapinduzi Balama, Zaeadi Mauya na Said Juma Makapu.

 

Kama Kaze ataamua kumtumia kama namba nane, Niyonzima anaweza kuwa katika eneo la namba 10 kama kocha ataamua kumtumia.

 

Balama alitumika kama namba 10 na kocha wa zamani, Luc Eymael, akiwa nyuma ya mshambuliaji mmoja katika mfumi wa 4-2-3-1, lakini sasa italazimika kubadili mfumo.

 

Kocha Kaze, ambaye aliwahi kuwanoa vijana wa Barcelona (Academy), anaweza kwenda na mfumo wa 4-3-3, mfumo ambao umekuwa maarufu kwa sasa kwa makocha wengi, badala ya ule wa 3-4-3, ambao unatumia zaidi ‘wing backs’.Toa comment