Kwa Rekodi Hizi…Simba Wataibatiza Coastal Kwa Moto leo Taifa

REKODI zinadumu bhana! Ndivyo unaweza kusema, hii ni baada ya Simba kuonekana mbabe mbele ya Costal Union ambayo watacheza nayo leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo wa ligi kuu.

 

Simba kwa sasa wako nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17, Coastal Union wenyewe wapo nafasi ya tatu na alama zao 30, wamecheza mechi 17 kama wapinzani wao.

Sasa rekodi zinaonyesha kuwa kwa msimu uliopita wa 2018/19 ambao Coastal Union ilipanda daraja, iliambulia kichapo mechi zake zote mbele ya Simba jambo linaloufanya mchezo wa leo kuwa mgumu.

 

Mchezo wa kwanza uliopigwa Dar kwenye Uwanja wa Uhuru ulishuhudiwa Simba ikiichakaza Coastal mabao 8-1 na ule uliochezwa Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani, Simba wakashinda tena kwa mabao 2-1.

 

Jumla Coastal Union imefungwa mabao 10-2 na kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, wachezaji wawili walifunga hat trick kutoka Simba ambao ni Emanuel Okwi na Meddie Kagere.

 

Sven alisema kuwa anahitaji kuona wachezaji wakipambana kupata pointi tatu, huku Juma Mgunda wa Coastal Union akisema.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka
Toa comment