Lamata Afunguka Harmo Kumtoa Machozi!

13 0

Lamata Afunguka Harmo Kumtoa Machozi!

KWA mara ya kwanza, sura yake ilionekana runingani mwaka 2008. Alikuwa na Kundi la Amka, wakiwa na tamthiliya yao matata ya Ndoano, iliyoruka kupitia Televisheni ya ITV.

 

Huyu ndiye Leah Richard Mwendamseke almaarufu kama Lamata, mzaliwa wa jijini Mbeya.

Ni bonge moja la mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, zijulikanazo kama Bongo Movies. Kwa sasa ndiye muandaaji na muongozaji wa Tamthiliya ya Kapuni inayoruka kupitia Televisheni ya Maisha Magic kwenye DStv.

 

Baadhi ya filamu alizoigiza na kuongoza ni pamoja na Kigodoro, Gumzo, Figo, After Death, My Princess, Tikisa, Mr & Mrs Sajuki, Poor Minds, Pain Killer, Time After Time, Mens Day Out, Confusion, All About Love, Last Minutes na nyingine kibao akiwa na mastaa wote unaowajua wa Bongo Movies.

 

Kwa zaidi ya miaka kumi kwenye Bongo Movies, Lamata ana mengi ya kushea na mashabiki wake. Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linamleta Lamata kwenye ukurasa huu ambapo mbali na mambo ya filamu, pia atafunguka sababu ya kuangua kilio hivi karibuni kutokana na kile alichofanyiwa na staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’, ungana naye;

 

IJUMAA WIKIENDA: Ukiacha waigizaji wanaojulikana, Tamthiliya ya Kapuni inazalisha vipaji vingi vipya na wamekuwa wanakusifia. Je, unajisikiaje?

LAMATA: Ninafurahi na kumshukuru Mungu, kama nimeweza kumtoa mtu chini na kumfikisha kwenye ustaa, binafsi ninapata faraja sana.

 

IJUMAA WIKIENDA: Unaweza ukakumbuka umeongoza filamu ngapi wewe mwenyewe na zikafanya vizuri sokoni?

LAMATA: Ni nyingi sana. Kuna My Angel, Rude, My Princess, Tears Forever, Time After Time, Dunia Nyingine, House Maid na sasa Kapuni na nyingine nyingi.

IJUMAA WIKIENDA: Wewe kama mwanamke, ni changamoto gani unazozipitia?

LAMATA: Hakuna kazi isiyokuwa na changamoto. Mimi naamini mtu ukipata changamoto, ni kitu kizuri kwa sababu zinakufanya uwe imara na uongeze juhudi zaidi.

IJUMAA WIKIENDA: Panapo changamoto lazima mafanikio yawepo, kwako ni mafanikio gani umeyapata hadi sasa?

 

LAMATA: Mafanikio ni ya kawaida tu kwa sababu mimi siangalii pesa. Kinachonifurahisha ni kukuza watu wenye vipaji.

IJUMAA WIKIENDA: Kwenye kila kazi lazima kunakuwa na mtu ambaye alikusapoti hadi kufika hapo ulipo, je, ni nani?

 

Lamata: Kwanza ni ujasiri wangu mwenyewe wa kutaka kujua. Wapo watu walionisapoti kama Ray (Vincent Kigosi) Seles Mapunda na Adamu Kuambiana (marehemu).

IJUMAA WIKIENDA: Juzikati tulimuona Harmonize kwenye bethidei yako, vipi uhusiano ukoje maana wananzengo wameanza kuhoji ukaribu wenu!

 

LAMATA: Harmonize tunafahamiana tangu anaingia kwenye muziki. Mimi ndiye nilikuwa naye wakati anaanza hadi leo tunafanya naye kazi pamoja.

IJUMAA WIKIENDA: Nini kilitokea hadi ukajikuta unamwaga machozi mbele yake?

 

LAMATA: Ile surprise aliyonifanyia ya kunimwagia pesa nyingi ilikuwa kubwa ambayo sikutarajia wala sikutegemea. Niliona ni upendo wa ajabu mno kwangu na nina thamani kubwa kwenye maisha yake. Yale yalikuwa ni machozi ya furaha niliyopata ndani yangu.

 

IJUMAA WIKIENDA: Vipi suala lake la kujitoa WCB, wewe kama mtu wake wa karibu ulilichukuliaje?

LAMATA: Kiukweli hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu lipo chini ya menejimenti yake.

IJUMAA WIKIENDA: Je, tangu ajitoe Wasafi, unaonaje mafanikio yake? Anapanda au anashuka kimuziki?

 

LAMATA: Tangu nilipofahamiana naye, nilijua atakuja kufanya mambo makubwa sana kwenye muziki kwa sababu ana kipaji kikubwa. Nadhani utabiri wangu unafanya kazi hadi sasa kwa sababu anazidi kupanda juu na ninafarijika kwa hilo.

 

IJUMAA WIKIENDA: Unawashauri nini mastaa wanawake wa Bongo Movies?

LAMATA: Wajitokeze kwa wingi, wawe waongozaji, madairekta, maprodyuza wa filamu na wapigapicha, wasihofie watapokelewaje kwenye tasnia hii kwa sababu mwanamke ukithubutu unaweza, yangu ni hayo tu!

Makala: Khadija Bakari
Toa comment

Posted from

Related Post

Sheva Apewa Kibaiskeli Simba SC

Posted by - March 19, 2020 0
Sheva Apewa Kibaiskeli Simba SC March 19, 2020 by Global Publishers Miraji Athuman ‘Sheva’ KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *