Linah: Inaniumiza Kulea Mtoto Mwenyewe

MWANADADA kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, amefunguka kuwa inamuumiza sana kumlea mtoto wake akiwa mwenyewe.

 

Akizungumza na Amani, Linah amesema kuwa kama mzazi, inamuumiza sana kulea akiwa peke yake, kwa sababu muda mwingine mtoto anahitaji kuwa karibu na baba yake, hiyo inamuathiri sana mtoto katika ukuaji wake.

“Kulea mtoto nikiwa peke yangu inaniumiza sana, maana mtoto anaweza akaamka akamuhitaji baba yake, na muda huo baba hayupo, hiyo inaniumiza sana kwa mtoto wangu, na inaniathiri hata katika muziki wangu maana naelemewa na majukumu,” alisema Linah.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA, AMANIToa comment