Lukaku Aandika Waraka Kwa Mashabiki Inter Milan

STRAIKARomelu Lukaku, ameandika waraka kwa mashabiki wa timu yake ya Inter Milan akisisitiza kuwa atarejea kwa kishindo baada ya bao lake la kujifunga kuigharimu timu hiyo kukosa taji la Europa dhidi ya Sevilla.

 

Straika huyo wa zamani wa Manchester United alifunga bao katika fainali hiyo na kuendeleza ubora wake lakini zikiwa zimebaki dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika na matokeo yakiwa 2-2, Lukaku alijifunga.

Mbelgiji huyo aliumia sana kiasi cha kushindwa kwenda kuchukua medali yake ya mshindi wa pili.

 

Lakini sasa katika posti yake ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii tangu fainali ile, Lukaku amewaahidi mashabiki wake kuwa atarejea kwa kishindo.Lukaku aliandika kwenye Instagram: “Kwanza napenda kuwashukuru wote kwa kile mlichokifanya kwa familia yangu na kwangu mwenyewe.

 

“Mwaka huu kama timu tumekua pamoja na ni heshima kuiwakili-sha klabu niliy-oipenda tangu nilipokuwa mtoto.“Ndiyo, kilichotokea kwenye fainali kilinihuzunisha lakini nitapambana tena.

 

“Hakuna kitu rahisi katika maisha kama wengi mnavyojua na uzoefu huu utanifanya niwe imara zaidi.

 

“Kitu kimoja ni uhakika kwamba Inter haijafa na uzoefu huu utatuboresha zaidi kama timu! Kuna umoja na tunaelekea katika mwelekeo sahihi.

 

“Kwa mashabiki, nataka kusema asanteni kwa kuendelea kutuunga mkono kila mechi nyumbani na ugenini, nawapenda sana.“Nazielewa meseji nilizozipata. Tutarejea kwa kishindo.”Toa comment