Lyyn Afichua Siri Utajiri Wake

11 0Lyyn Afichua Siri Utajiri Wake

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Irene Louis ‘Lyyn’ ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘maneno’, amefunguka siri za utajiri wake kuwa ni mali alizoachiwa na wazazi wake na siyo kwamba amezipata kwa kudanga.

 

Mrembo huyo ambaye amekuwa akionekana kula bata kupita maelezo huku akiishi kwenye ghorofa la kifahari na kutembelea ndinga kali zaidi ya moja, aliendelea kueleza kwamba juhudi zake pia zimemfikisha hapo alipo, huku akipuuza uvumi kuwa amekuwa akiendesha maisha yake kwa kuhongwa na wanaume.

 

Mmoja kati ya wambeya wa mtandaoni aliandika hivi karibuni kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Huyu Lyyn ni mdogo sana lakini anaishi maisha ya kifahari kama siyo kudanga huku ni nini?”

 

Kufuatia sarakasi za huko mitandaoni kumhusu msanii huyo, RISASI lilimtafuta mrembo huyo na kufanikiwa kufanya naye mahojiano maalumu kuhusu maisha unayoishi, baadhi ya watu wanadai mali zote unazomiliki ni kwa sababu ya kudanga, hili lina ukweli kiasi gani?

 

LYYN: (Anacheka) Unajua ambapo alifunguka mambo mengi usiyoyajua toka kwake.

RISASI: Mambo Lyyn?

LYYN: Poa tu

RISASI: Kumekuwa na maneno mengi yanasemwa juu yako, watu wengi wanapenda sana kumjaji mtu kwa nje, ila hawajui hata robo ya maisha yake ilivyo.

RISASI: Kama hautojali unaweza kutuambia kidogo hayo magari na nyumba za kifahari unazoishi pesa unatoa wapi?

LYYN: Sisi kwetu tulizaliwa watoto kumi na mimi ndiyo mtoto wa mwisho, wazazi wangu walifariki nikiwa bado mdogo hivyo kuna nyumba ambazo tuliachiwa, sasa ukianza kupiga mahesabu tangu kipindi kile nipo mdogo mpaka sasa nimekuwa unaona ni pesa kiasi gani ambazo nakuwa nazo kwenye akaunti yangu, kwa sababu kipindi nipo mdogo nilikuwa sizitumii, lakini baada ya kukua ndio nimeanza kuzitumia.

 

“Nina magari manne ambayo ni BMW, Jaguar, Volkswagen na Mark X, lakini pia nina nyumba zaidi ya mbili zipo Kigamboni zote nimepangisha kuna watu wanaishi, hivyo nakuwa nachukua tu kodi, kwa hiyo ifike mahali watu waache kumsema mtu kwa ajili tu ya muonekano wake, kwa sababu mbali na kazi ya sanaa nina vitu vyangu vingine nafanya ila sipendi kuvionyesha hadharani.

 

Mara kadhaa vyombo vya habari mbalimbali vimekuwa vikimtaja mrembo huyo kuwa ni miongoni mwa wasanii ambao wanaishi kwa kula bata mjini ambapo leo ufafanuzi wa jeuri ya fedha aliyonayo umetolewa na sisi tunatua mzigo jamvini, karibu kwa mjadala mwingine. 

 

STORI MEMORISE RICHARD, RISASI
Toa comment

Posted from

Related Post

Wakenya waonja Joto la Jiwe

Posted by - May 22, 2020 0
Wakenya waonja Joto la Jiwe May 22, 2020 by Global Publishers MVUTANO kuhusu uamuzi wa Serikali ya Kenya kufunga mipaka…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *