Mabadiliko ya Yanga Yaiva, Senzo Aanza Kazi Rasmi – Video

KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi al;iyekuwa CEO wa Simba SC, Senzo Mazingisa kuwa mshauri wao ambapo atashirikiana na uongozi wa klabu na GSM kwenye mazungumzo ya mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo wakishirikiana na La Liga na Sevilla, kuanzia.

 

Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla amemtambulisha Senzo mbele ya wanahabari na kusema kuwa sasa kazi ya kuubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo unaanza rasmi.

 

“Yanga SC tumemchukua Senzo kama mshauri wetu hasa kwenye haya mabadiliko tunayokwenda kuyafanya. Tunao washauri wa La Liga na Sevilla, tumeona na yeye tumuongeze sababu ana rekodi nzuri ya uongozi wa masuala ya Soka, ameshaanza kushiriki vikao vyetu,” amesema Dkt. Msolla.

 

Kwa upande wake, Senzo amesema;

“Si kazi rahisi kujiunga na Yanga SC kwa sababu ni moja ya klabu kongwe, kubwa na yenye historia nzuri Barani Afrika. Kwangu ni bahati, nitafanya kazi ya kuishauri klabu na kuhakikisha tunaingia kwenye mfumo mpya, wa kisasa kuiongoza klabu ili kuwa tayari kushindana.

 

“Nitakuwa mshauri na kiunganishi kati ya La Liga & Sevilla pamoja na Yanga SC, nitatoa ushirikiano wangu wote kwa kushirikiana na viongozi wa Klabu pamoja na GSM kuleta mafanikio ndani ya Klabu, sasa najisikia mwanafamilia wa Yanga SC.



Toa comment