Mabaki ya samaki maarufu wa Zambia ‘Mafishi’ yatoweka

1 0

Mabaki ya Mafishi – samaki maarufu wa Zambia ambaye kifo chake kimeombolezwa tangu Jumatatu – yametoweka mahali iliyokuwa imehifadhiwa. Samaki huyo aliishi kwenye kidimbwi cha Chuo Kikuu cha Copperbelt (CBU) kwa zaidi ya mwongo mmoja na wanafunzi walimchukulia kama chanzo cha bahati.

Aliombolezwa na viongozi wakuu serikalini akiwemo rais Edgar Lungu na baadhi ya mawaziri wake.

Naibu Chansela wa CBU Naison Ngoma, amethibitisha kutoweka kwa mabaki ya mafishi na kuongeza kuongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichotokea, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Zambia Daily Mail.

“Nalifahamishwa kwamba samaki huyo alianza kutoa harufu mbaya kwenye jokovu Iakini nilipoulizia yuko wapi niliambiwa ametoweka’’alinukuliwa kusema.

Kwa mujibu wa BBC. Prof Ngoma anasema huenda samaki huyo ameliwa au kutupwa. Ameongezea kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wale waliohusika na kutoweka kwa samaki huyo.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *