Mafuriko ndani ya nyumba ya Jacqueline Mengi (+Video)

20 0

Mjasiriamali Jacqueline Mengi amesimulia namna mvua ilivyoweza kusababisha mafuriko nyumbani kwake na kuleta uharibifu na hasara kubwa.

Jacqueline Mengi kupitia Video fupi ameonesha namna vitu mbalimbali vilivyoweza kuharibiwa na mafuriko hayo huku akieleza namna hali ilivyokuwa.

”Hii ndiyo nyumba yangu baada ya mafuriko, uharibifu mkubwa na hasara. Hizi Video zinaonyesha sehemu ndogo tu ya uharibifu tuliopata.”

Mjasiriamali huyo amesema baada ya kutokea kwa hali hiyo aliangua machozi na kukata tamaa na katika hali hiyo inaweza kumtokea mtu yoyote yule.

Ameongeza kuwa sababu ya kulia ni kuwa kati ya vitu vingi alivyopoteza kutokana na mafuriko hayo vinathamani kubwa katika hisia, ni vitu ambavyo vinamkumbusha yeye binafsi na watoto wake kuhusu baba yao. Na vingi kati ya hivyo vitu vilikuwa ni zawadi ambazo zimebeba kumbukumbu nyingi.

”Nikiwa sakafuni nalia mapacha wangu walikuja na kunikumbatia, wakijaribu kunifariji na kuanza kuomba, katika sala walimshukuru Mungu kwamba bado tuko hai na hakika iliniuma.”

Jacqueline Mengi ameendelea kwa kusema wamepoteza vitu vingi na kamwe havina mbadala wake lakini bado wana mengi ya kushukuru na walau wanakumbukumbu zilizohifadhiwa ndani ya myoyo yao na akili. Amemalizia kwa kusema anafahamu kuwa wapo watu wengi wameathiriwa na mafuriko, anawapa pole kwa hasara walizopata kwakuwa anatambua maumivu yalivyo lakini amewakumbusha kushukuru kwakuwa bado wanaishi na Mungu wabariki wote.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *