Magufuli Aeleza Kitwanga Alivyomsumbua Ujenzi wa Barabara -Video

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Pombe Magufuli, amekumbuka jinsi ambavyo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga alivyokuwa akimsumbua kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Usagara, ambayo hapo mwanzo haikuwepo.

Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga.

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 8, 2020, wakati akizugumza na kumnadi mgombea wa sasa wa Jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti katika eneo la Usagara.

“Mimi nataka tu nieleze ukweli, nilikuwa na Mbunge hapa Mh Kitwanga alikuwa ananisumbua sana, baadhi ya miradi nataka kuwaeleza mipango iliyofanyika hapa ni mingi hata hii Barabara haikuwepo katika kipindi cha miaka mitano tuliifanya na aliyenisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni alinisumbua sana ujenzi wa barabara hiyo”, amesema Rais Magufuli.Toa comment