Magufuli; Katambi ni Kijana Nampenda Mpeni Kura, Atawavusha -Video

1 0Magufuli; Katambi ni Kijana Nampenda Mpeni Kura, Atawavusha -Video

MGOMBEA Urais wa CCM, Ndg John Magufuli leo  Septemba 03, 2020 amezungumza na Wananchi wa Shinyanga mjini katika Mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga

Akiongea na wananchi hao amesema aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu Stephen Masele atamtafutia kazi nyingine.

“Yale mengine ya pembeni achaneni nayo, Katambi ni kijana nampenda mpeni kura, atawavusha, jana tu nimekutana na Masele aliyekuwa Mbunge wa hapa wala sina tatizo, mimi ni Rais nitamtafutia kazi nyingine, ukishakuwa Rais Makazi yapo mengi tu”-JPM akiwa Shinyanga

Katika kampeni hizo Magufuli amesindikizwa jukwaani na Linah Sanga, Young Dee, Msechu, Bob Haisa, Mrisho Mpoto, Banana Zorro, Chege na Sholo Mwamba.

Aliyoyasema Mgombea Urais CCM Rais Dkt. Magufuli;-

“Hadi Sasa Tumetumia Bilioni 29.9 Kwa ajili ya Utoaji Elimu Bila Malipo. Kiasi cha Shilingi Bilioni 60 tulizielekeza kwenye Utekelezaj wa Miradi Mbalimbali ya Maji. Katika miaka mitano iliyopita tumehangaika wote na Mengi tumeyafanya, Naombeni Kura Zenu Wana Shinyanga”

“Tutakarabati uwanja wa ndege wa Shinyanga na Sumbawanga, fedha zipo na tenda zimetangazwa, badala ya kwenda kupanda ndege Mwanza, mtapandia hapahapa na hili lipo kwenye Ilani ya CCM na nawahakikishia lazima tufanye”

“Hapa Shinyanga tumeteleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Hospitali, Zahanati, tumekamilisha mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Iringa-Dodoma-Singida hadi Shinyanga, itafika mahali tatizo la umeme litakuwa ni ndoto, vijiji 136 vya Mkoa huu tumepeleka umeme”

“Kuna malalakiko ya kutokukamilika kwa barabara ya Ndala, TANROADS walete bajeti, fedha nitazitoa kwa ajili ya barabara hii, wewe Katambi ukichaguliwa hii ndiyo kazi yako ya kwanza kunikumbusha, usije ukachaguliwa ukajisahau”Toa comment

Posted from

Related Post

KICHUYA ARUDI NA UTAMU WAKE

Posted by - June 12, 2020 0
NA WINFRIDA MTOI WINGA wa Simba, Shiza Kichuya, ameanza kurejea katika utamu wake baada ya juzi kupiga soka la kiwango…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *