Magufuli: Tizeba Njoo Umuombee Kura Shigongo – Video

5 0Magufuli: Tizeba Njoo Umuombee Kura Shigongo – Video

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama hicho, Dkt. John Magufuli amemtaka aliyekuwa mbunge wa jimbo la Buchosa aliyemaliza muda wake, Dkt. Charles Tizeba kusimama na kumuombea kura Eric Shigongo ambaye anagombea ubunge wa jimbo hilo kwa sasa.

 

Magufuli amesema hayo leo Jumanne, Septemba 8, 2020, wakati akizungumza na wananachi wa Bukokwa na Nyehunge, mkoani mwanza wakati akiendelea na kampeni zake huku akimpongeza Tizeba kwa kazi kubwa aliyofanya kwa miaka 10 na kuahidi kumpa kazi nyingine Serikalini.

 

“Mambo makubwa yaliyofanyika Buchosa kwa miaka mitano tunasema asante sana Mhe. Rais, umetupatia Hospitali ya Wilaya, sasa kazi yako Shigongo tekeleza, songa mbele, wananchi wa Buchosa tumpe kura Shigongo, wafuasi wa Tizeba mliokuwa mnanuna ole wenu niwaisikie.

 

“Mimi nimefanya miaka 10, Shigongo aombe mitano akimaliza aombe mingine iwe 10 kama itampendeza Mungu, uongozi ndivyo ilivyo, sisi wazalendo wa kweli kazi hutii mamalaka ya wananchi na chama, nawaombeni tumpe ushirikiano Shigongo, nilipofikia mimi naye asonge mbele,” amesema Dkt. Tizeba.

 

kwa upande wake Shigongo amesema; “Sote tunafahamu mambo ambayo Mhe. Rais Magufuli ameyafanya Buchpsa, mambo ambayo Dkt. Tizeba ameyafanya, nitaanzia alipokomea Tizeba kwenda mbele.”

 

“Mhe. Rais mimi kijana wako ninakuomba uwakumbuke watu wa Kome uwajengee kivuko, tukumbuke hii Barabara ya Sengerema – Nyehunge mpaka Kahunda ijengwe kwa lami, nilipita hapa watoto wadogo wakanisimamisha wanataka lami, una moyo wa kuwapenda watu, tukumbuke BABA,” amesema Shigongo.

 

Aidha, Magufuli amewataka wananchi wa Buchosa kuvunja makundi yao na kumchagua Shigongo na madiwani wa CCM ili wakapige kazi huku akiahidi kujenga barabara ya Sengerema – Nyehunge kwa kiwango cha lami kabla ya Desemba mwaka huu.

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *