Mama Samia Awapokea Wanachama 150 wa Upinzani Tandahimba

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM ya 2020/25 Mbunge mteule kwa tiketi ya CCM Jimbo la Mahuta Tandahimba Katawi Ahmad Katawi kwa ajili ya kuinadi kwenye mikutano ya Kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM leo Septemba 11,2020.

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Ndugu Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 11, 2020 amefika kuwahutubia Wananchi wa Jimbo la Mahuta Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara  kwenye Mkutano wa Kampeni wa CCM katika Uwanja wa Kijiji cha Mahuta Mtwara leo Septemba 11, 2020.

Jumla ya wanachama 150 kutoka vyama vya ACT, CUF na Chadema wilayani Tandahimba warudisha kadi zilizokuwa za Vyama walivyotoka baada ya kujiunga na CCM kwenye Mkutano wa huo wa Kampeni.

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Jimbo la Mahuta Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara baada ya kuwahutubia mkutano wa Kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Mahuta Tandahimba Mtwara leo Septemba 11, 2020.

Jumla ya Wanachama 150 kutoka Vyama ACT Wazalendo, CUF na Chadema Wilayani Tandahimba wakionesha na kurudisha kadi zilizokuwa za Vyama walivyotoka baada ya kuamuwa kuvihama Vyama hivyo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM kwenye mkutano wa Kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo Septemba 11,2020 katika Uwanja wa Mahuta Wilayani Tandahimba ambapo Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwapokwa Wananchi hao.Toa comment