Mamba aliyepata umaarufu India, baada ya kuonekana akiwapa ulinzi wa kipekee watoto wake

1 0

Picha inayomuonesha mamba akiwabeba watoto wake mgongoni kwa kutumia mbinu isiokuwa ya kawaida inaendelea kuzua gumzo mitandaoni.

Picha hiyo ya kuvutia ilinaswana mpicha Dhritiman Mukherjee katika hifadhi ya Uttar Pradesh nchini india.

Miito imekuwa ikitolewa kupendekeza mpiga picha huyo apewe tuzo ya mwaka huu ya picha bora ya wanyhama pori.

Dhritiman anasema mamba kwa kawaida huwabeba watoto wao kwa (makini) wakitumia mdomo, lakini mbinu iliyotumiwa na mamba huyu ni ya kustaajabisha na ni vigumu kwake kuwapa ulinzi watoto.

“Ili kujiokoa watoto walilazimika kujishikilia katika eneo la kichwa cha mama na hata wengine kupanda mgongoni ili kuwa salama,” anasema.

Thuluthi tatu ya mamba hao wanapatikana katika hifadhi ya Uttar Pradesh, hali ambayo huenda ikawa jambo la muhimu kwa mamba wadogo kujilinda kwa njia isiokuwa ya kawaida wanapobebwa na mama zao.

Chanzo BBC.

Posted from

Related Post

WINGA MSUMBUFU YANGA NI HUYU

Posted by - September 4, 2019 0
NA MWAMVITA MTANDA UNAMKUMBUKA yule winga wa Yanga, Simon Msuva, jinsi alivyokuwa akiwasumbua mabeki hapa nchini? Basi habari njema ni…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *