Mambo 6 Miaka 30 ya Wema

MSANII na nyota wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu siku ya leo Septemba 29 anatimiza miaka 30, ambapo kupitia instagram yake amepost picha mbalimbali zikimuonesha kujipongeza, haya hapa ni mambo sita ya kufahamu kuhusu siku yake hii muhimu ya kuzaliwa.

 

1. Wafuasi ‘followers’ wengi instagram

Wema Sepetu ndiye msanii wakike mwenye wafuasi wengi kuzidi wasanii wengi wa kike Bongo ambapo ana followers milioni 7.7 huku akiwa ame-follow watu 515, hii inatokana umaarufu wake na kupendwa na watu wengi.

2 .Miss Tanzania 2006

Wema Sepetu alivishwa taji hilo mwaka 2006 baada ya kuwashinda warembo kama Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, na Lisa Jensen ambao walifika tatu bora katika kumtafuta mrembo bora Tanzania.

3. Tuzo ya msanii bora wa kike

Wema amewahi kuchukua tuzo ya sinema zetu Aprili 2018, aliipata tuzo hiyo kupitia kinyang’anyiro cha ‘Peoples Choice’ wakati wa kumchagua muigizaji bora wa kike na kuwashinda waigizaji kama Riyama Ally na Rachel Kayuga.

4.Orodha ya wapenzi aliowahi kutoka nao

Inasemekana kuwa Wema Sepetu ni miongoni mwa msanii wa kike ambaye amewahi kutoka na wasanii maarufu nchini kama vile marehemu Steven Kanumba, Idris Sultan, Bob Junior, Mr. Blue, TID, Calisah na wengine wengi na baadaye kuachana nao.

5. Kukosa mtoto

Moja kati ya vitu vinavyomtesa Wema Sepetu ni kukosa mtoto na kwa bahati mbaya sana watu wengi wamekuwa wakitumia udhaifu huo kumshambulia mitandaoni ila binafsi anaamini ipo siku atapata mtoto wake mwenyewe na kumlea.

6. Kupunguza mwili

Watu wamekuwa wakimhukumu kuhusu muonekano wake wa sasa ambapo wanasema anachukiza, amepoteza mvuto na kuonekana kama amekonda baada ya kufanya surgery ya kupunguza baadhi ya nyamanyama za mwili wake ambazo zilikuwa zinamfanya aonekane ana mwili mkubwa.
Toa comment