Mambosasa aeleza jinsi majambazi wawili walivyouawa Dar (+Video)

8 0

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limekamata Bastola mbili na kuwaua majambazi wawili katika matukio mawili tofauti.

Kamanda Mambosasa

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema mmoja wa majambazi ameuawa katika eneo la Mbagala Zakheim ambapo alikuwa na wenzake watatu wakijiandaa kuvamia maduka ya miamala ya fedha.

Jambazi wa pili aliuawa katika eneo la Shekilango baada ya majambazi kujaribu kuwashambulia askari waliokuwa doria wakiwafuatilia hivyo katika kujihami maaskari wakafanikiwa kumpiga risasi mgongoni.

Aidha Mambosasa ameeleza silaha walizozikamata ni Bastola mbili moja ikiwa na risasi tano huku ikiwa imetengezwa nchini Brazil.

View this post on Instagram

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limekamata Bastola mbili na kuwaua majambazi wawili katika matukio mawili tofauti. Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema mmoja wa majambazi ameuawa katika eneo la Mbagala Zakheim ambapo alikuwa na wenzake watatu wakijiandaa kuvamia maduka ya miamala ya fedha. Jambazi wa pili aliuawa katika eneo la Shekilango baada ya majambazi kujaribu kuwashambulia askari waliokuwa doria wakiwafuatilia hivyo katika kujihami maaskari wakafanikiwa kumpiga risasi mgongoni. Aidha Mambosasa ameeleza silaha walizozikamata ni Bastola mbili moja ikiwa na risasi tano huku ikiwa imetengezwa nchini Brazil. (📹 via Eatv.tv)

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on Jun 27, 2020 at 4:39am PDT

The post Mambosasa aeleza jinsi majambazi wawili walivyouawa Dar (+Video) appeared first on Bongo5.com.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *