Manara: Yanga SC Watakutana na Balaa la Bwalya, Miquissone

UONGOZI wa Simba umesema kuwa mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo inatarajiwa kupigwa Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa imepangwa mapema sana jambo ambalo linawapa hasira ya kujipanga vizuri.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa alipoona ratiba alishangaa kwa kuwa wao wameshakiweka kikosi tayari na wapo tayari kwa ushindani huku akisisitiza kuwa wapinzani wao hao watakutana na balaa la nyota kama Larry Bwalya na Luis Miquissone.

 

“Wale wenzetu tunakutana nao Oktoba 18 mwaka huu kwenye ligi, dah! Itakuwa balaa, mbona wametufanya tukutane mapema, yaani sijui itakuwaje, maana hilo mbungi litakalopigwa siyo la nchi hii.

 

“Fikiria una mtu kama Bwalya (Larry), Miquissone (Luis), Chama (Clatous) hapo ujue wengine sijawataja mimi sijui itakuwaje, ila tusubiri na tuone,” alisema Manara.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es SalaamToa comment