MAREKANI: Leo ndio kumbukumbu ya miaka 18 ya shambulio la septemba 11, lililosababisha vifo vya watu 3000 – Video

20 0

Septemba 11, 2001 ni tarehe inayokumbukwa kwa shambulizi baya kuwahi kufanyika Marekani na kusababisha vifo vya watu takribani 3,000 na kujeruhi wengine 6,000 baada ya kundi la kigaidi la Al-Qaeda kuteka ndege nne.


Kundi hilo likiongozwa na Osama bin Laden waliziteka ndege hizo ambapo ndege ya kwanza iliyokuwa ikitokea Boston, ililazwa kwenye mnara wa Kaskazini wa Kituo cha Biashara Ulimwenguni jijini New York.Ndege ya pili, pia kutoka Boston, iligonga mnara wa Kusini dakika 17 baada ya ile ya kwanza. Ndege ya tatu ikitoka Uwanja wa Ndege wa Dulles iligonga upande wa Kusini Magharibi wa Pentagon.

Ndege ya nne kutoka Newark, New Jersey, iligonga karibu na Shanksville mashambani mwa Pennsylvania baada ya abiria kupata habari ya matukio na kujaribu kuwashambulia watekaji.


Tangu shambulio hilo kutokea, Marekani walikuwa wakimsaka kiongozi wa kundi hilo Osama Bin Laden na kufanikiwa kumuua May 2, 2011 na Marekani imekuwa ikipunguza vikosi vyake nchini Afghanistan tangu Osama alipouawa.

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *