Marekani: Moto mkubwa waibuka California, helkopta zatumika kuokoa watu

12 0

Moto mkubwa wa mwituni uliyoambatana na joto kali umeangamiza zaidi ya kilomita 8000 za mraba katika jimbo la California nchini Marekani.

Wizara ya misitu na ulinzi dhidi ya moto nchini humo imesema huu ndio moto mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1987.

Kusini mwa jimbo la California, wakazi walishauriwa kuziacha nyumba zao zinazonyemelewa na moto huo na kutafuta hifadhi mahali salama.

California wildfires: Helicopter crews rescue at least 35 more who were  trapped by Creek Fire - CNN

Upande wa kaskazini wa jimbo hilo, watu wapatao 200 waliokolewa na helikopta za kijeshi, baada moto huo kuuzingira kwa kasi mji wa Fresno.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *