Mason Greenwood aungana na Phil Foden kuomba msamaha kwa kosa la kuingiza wanawake kambi ya timu ya taifa

4 0

Mshambuliaji wa kikosi cha England Mason Greenwood amesema ” yeye mwenyewe ndiye wa kulaumiwa” baada ya kuondoshwa kwa kosa la kukiuka muongozo wa karantini kutokana na virusi vya corona huko Iceland.

Mchezaji huyo wa Manchester United na Kiungo wa kati wa Manchester City Phil Foden, waliamriwa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Gareth Southgate siku ya Jumatatu.

Greenwood alisema: “Ninaweza tu kuomba msamaha kwa aibu niliyoisababisha.”

Aliongeza: ”Hususani , ninataka kumuomba radhi Gareth Southgate , kwa kumuangusha, wakati alionesha kuniamini kwa kiasi kikubwa.

”Kuichezea England ilikuwa moja kati ya nyakati za kujivunia sana katika maisha yangu na ni mimi pekee ninayepaswa kulaumiwa kwa kosa hili kubwa.

”Ninaiahidi familia yangu, mashabiki, Manchester United na England kuwa hili ni somo nitajifunza.”

Kwa mujibu wa ripoti za Iceland na vyombo vingine, Foden na Greenwood walidaiwa kukutana na wanawake wawili katika sehemu tofauti za hoteli mbali na mahali kikosi cha England kilipokuwa kinakaa.

Southgate amewaelezea wachezaji hao kuwa ‘wajinga’ akiongeza kuwa : ”ni suala kubwa sana na tumelishughulikia namna hiyo na tumechukua hatua haraka sana kadiri tulivyoweza”.

”Tumelishughulikia ipasavyo. Ninatambua umri wao lakini dunia nzima inashughulika na janga hili.”

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *