Maxime: Nina Mkataba wa Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefunguka kuwa alipewa mkataba wa kujiunga na Yanga, lakini kutokana na kutofi kia baadhi ya makubaliano, alishindwa kuusaini na mpaka leo bado anao.

 

Maxime aliyewahi kuifundisha Mtibwa Sugar, amesema alipewa mkataba huo Desemba mwaka jana kipindi ambacho Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha wa muda, Charles Mkwasa akisaidiwa na Said Maulid ‘SMG’.

 

“Ni kweli nina mkataba wa Yanga ambao walinipa tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini sijausaini kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda sawa. Mimi bado ni mwajiriwa wa Kagera Sugar na mambo yakienda kama inavyotakiwa sina hiyana kujiunga na Yanga,” alisema Maxime.

 
Toa comment