Mbaroni kwa kumtumia barua ya sumu Rais Trump

1 0

Mwanamke huyo alikamatwa na maafisa wa marekani huku akiwa amebeba bunduki, hii ni kwa mujibu wa maafisa wa usalama.

Inadaiwa kifurushi kilichokuwa na sumu ya ricin ambacho kilitumwa kwa Rais Donald Trump kilizuiwa kabla ya kufika Ikulu ya White House, maafisa wameviambia vyombo vya habari vya Marekani.

Barua hiyo iligunduliwa katika kitengo cha ukaguzi wa vifurushi vya barua katika Ikulu ya White House mapema wiki hii , wanasema maafisa.

Walisema kuwa sumu hiyo iliyopatikana ndani ya bahasha ilitambuliwa kama ricin, sumu ambayo kwa kawaida hupatikana katika maharagwe.

Ricin hutengenezwa kwa kusindikwa kwa maharage ya castor . Ni sumu inayoua ambayo kama ikimezwa, kuivuta wakati wa kupumua au kuchomwa sindano yake , inaweza kusababisha kizunguzungu, kutapika, kuvuja damu ndani ya mwili na kusimamisha utendaji wa viungo vya ndani ya mwili.

Iwapo mtu atatumia sumu ya ricin, kifo chake kinaweza kutokea katika kipindi cha saa 36 na 72, kulingana na kiwango cha dozi iliyoingia mwilini mwake, kwa mujibu wa Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuwia magonjwa (CDC).

CDC kinasema sumu hiyo-ambayo imekwishawahi kutumiwa katika njama za ugaidi-inaweza kutengenezwa kuwa silaha katika muundo wa poda, au mvuke.

Posted from

Related Post

Mondi, Tanasha Tutawambia Nini Watu?

Posted by - February 17, 2020 0
Mondi, Tanasha Tutawambia Nini Watu? February 17, 2020 by Global Publishers TUTAAMBIA nini watu? Ndiyo msemo unaotumika huko mitandaoni baada…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *