Mbele ya JPM, Kigwangalla Asimulia Alivyouza Vitumbua, Jojo – Video

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla, amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliokulia katika mazingira ya kawaida na alikuwa akizunguka mitaa ya Nzega akiuza vitumbua na Jojo.

 

Ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 2, 2020, mjini Nzega Mkoani Tabora, alipokuwa akizungumza na wananchi wa mji huo, wakati mgombea urais wa chama hicho Dkt John Magufuli alipopita hapo kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi wa Nzega.

 

“Mimi nimezaliwa na kukulia katika viunga vya mji huu, ni mtoto wa kawaida kabisa kutoka familia ya kawaida kabisa ya Kiswahili.  Nimezunguka katika mitaa ya Nzega nikiuza vitumbua na Jojo, nikifanya shughuli za kawaida kabisa ambazo kwa kiasi kikubwa zinafanywa na wananchi ambao siku hizi wanaitwa wanyonge”, amesema Dkt Kigwangalla.

 

Awali alimshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kwa kumpa nafasi mbalimbali za uongozi serikalini ikiweno nafasi ya Naibu Waziri wa Afya, na nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii.

 Toa comment